RUWAZA YA VIVUMISHI KATIKA LUGHA AMBISHI BAINISHI: MIFANO KUTOKA LAHAJA YA KIIMENTI

Journal of Kiswahili and Other African Languages · Volume 1, Issue 1 (2022) · pp. XX–XX

DOI: 10.58721/jkal.v1i1.95

Abstract

<jats:p>Kivumishi ni kipashio muhimu katika lugha yoyote ile. Kinatumika pamoja na kategoria nyingine za maneno katika sentensi ili kufanikisha mawasiliano. Utafiti kuhusu kategoria mbalimbali za maneno umewahi kufanywa. Hata hivyo, hatujakumbana na utafiti unaoangazia ruwaza za kivumishi cha Kiimenti katika tungo za lahaja husika. Hivyo basi nia kuu ya makala haya ni kuthibitisha jinsi kivumishi katika lahaja hii hudhihirisha ruwaza mbalimbali kinapotumika katika sentensi za lahaja hiyo. Data iliyochanganuliwa na kuwasilishwa katika makala haya ilikusanywa maktabani na nyanjani. Maktabani tulirejelea kazi mbalimbali kuhusu ruwaza za vivumishi hasa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Aidha, tulisoma vitabu vya hadithi za Kiimenti ili kupata data ya kuchanganuliwa katika makala haya. Nyanjani tulikusanya data kutoka tarafa ya Abothuguchi ya Magharibi, kaunti ndogo ya Meru katika kaunti ya Meru.  Kwa kutumia sampuli maksudi tuliteua miktadha ya mikutano ya kanisa, shule, soko na ile ya chifu ambapo tulikusanya data. Tunatarajia kuwa makala haya yatasaidia katika uandishi wa sarufi ya lahaja ya Kiimenti na pia kuchangia katika uhifadhi wake ili kuendeleza usomi. Kwa sasa lahaja ya Kiimenti haina maandishi mengi na haijatiliwa maanani sana katika mfumo wa elimu nchini Kenya.</jats:p>